MKUTANO WA TANSHEP TAREHE 19 - 20 /12/2019

MKUTANO WA TANSHEP TAREHE 19 - 20 /12/2019

MKUTANO WA KUBADILISHANA UZOEFU WA MRADI WA TANSHEP UNAOTEKELEZWA MIKOA YA KILIMANJARO, ARUSHA NA TANGA

ENEO; KILIMAJARO RAS OFFICE HALL (MOSHI)

TAREHE; 19-20 DECEMBER, 2019

 

Mkutano uliwakutanisha wakulima (vikundi vya wakulima) wa mazao ya bustani kutoka mikoa ya Kilimanjaro, Arusha, Tanga, Mbeya, Iringa, Njombe na Morogoro na makampuni/wadau mbalimbali wa mnyororo wa thamani wa mazao ya bustani.

Ajenda ya mkutano ikiwa ni

  • kutoa taarifa ya mendeleo na mafanikio ya TANSHEP tangu ilipoanza kwenye mikoa mitatu ya awali
  • kujadili namna ya kuunda mahusiano endelevu baina ya wadau wa mnyororo wa thamani wa mazao ya bustani
  • kujadili na kufahamu shughuli za TANSHEP kwenye mikoa husika

 

Aidha mkutano uliweza kuwapa fursa wakulima hao wa mazao ya bustani kuweza kuzungumza na makampuni/wadau mbalimbali waliohudhuria mkutano huo kuhusu namna ambayo wakulima wanaweza kunufaika Zaidi na wadau hao muhimu katika suala la masoko, pembejeo na kuongeza uzalishaji kiujumla ili kuweza kufikia azma ya kauli mbiu ya TANSHEP isemayo “ANZIA SOKONI, MALIZIA SHAMBANI KWA KIPATO ZAIDI

Download File/s: