MRADI WA TANSHEP NA MAFUNZO YA KUONGEZA UWEZO KWA MAAFISA UGANI WA KILIMO

MRADI WA TANSHEP NA MAFUNZO YA KUONGEZA UWEZO KWA MAAFISA UGANI WA KILIMO

MRADI WA TANSHEP KATIKA MAFUNZO YA KUONGEZA UWEZO WA MAAFISA UGANI WA KILIMO KWENYE MIKOA INAYOTEKELEZA MRADI

 

Warsha katika mkoa wa Kilimanjaro kati ya mikoa mitatu ya utekelezaji wa mradi wa TANSHEP

 

Ili kuweza kufikia ubora wa mazao ya bustani yanayokidhi mahitaji ya soko ni lazima mkulima aweze kutambua na kudhibiti aina mbalimbali ya wadudu na magonjwa yanayoweza kushambulia mazao hayo kipindi cha uzalishaji.

 

Mradi wa TANSHEP umeendelea kuwajengea uwezo maafisa ugani juu ya kutambua na kudhibiti magonjwa na wadudu/visumbufu vya Mazao ya bustani (mfano nyanya, Tango, Kabichi, Pilipili hoho na karoti).

 

TANSHEP iliandaa warsha ya kutoa mafunzo kwa maafisa ugani katika mikoa ambayo inatekeleza mradi wa TANSHEP. Mafunzo hayo yakiwa na lengo la kuhakikisha wakulima kupitia maafisa ugani wa kilimo wanaweza kutatua changamoto za magonjwa na wadudu/visumbufu kwenye mazao ya bustani kipindi cha uzalishaji ili kuweza kupata mazao yenye kiwango na ubora unaohitajika sokoni.

 

Mafunzo hayo kwa maafisa ugani wa kilimo yalitolewa na wakufunzi kutoka chuo cha HORT-Tengeru katika wilaya mbili za kila mkoa wa utekelezaji wa Mradi wa TANSHEP (Kilimanjaro, Arusha, Tanga).

 

Katika mkoa wa Kilimanjaro mafunzo kwa maafisa ugani kilimo yalitolewa tarehe 17/03/2020 katika wilaya ya Moshi ambapo maafisa ugani takribani kumi na sita (16) walihudhuria na kupata mafunzo ya kuongeza uwezo wa utambuzi na udhibiti wa magonjwa na wadudu/visumbufu vya mazao ya bustani. Aidha, tarehe 18/03/2020 mafunzo yalitolewa katika wilaya ya Hai ambapo maafisa ugani takriban kumi na nne (14) walihudhuri na kupewa mafunzo hayo ya kuongeza uwezo.

 

Mafunzo haya ni miongoni mwa njia/mikakati ya mradi wa TANSHEP katika kuhakikisha Mbinu ya SHEP inakuwa ni yenye mafanikio makubwa kwa wakulima wa mazao ya bustani. Hii ikiwa ni katika namna ya kuendelea kuweka mkazo kwenye kauli mbiu isemayo "anzia sokoni malizia shambani kwa kipato zaidi".