Programu ya Kuendeleza Sekta ya Kilimo Awamu ya Pili - Lugha Nyepesi

Programu ya Kuendeleza Sekta ya Kilimo Awamu ya Pili - Lugha Nyepesi

Programu ya Kuendeleza Sekta ya Kilimo awamu ya Pili (Agricultural SectorDevelopment Programme phase Two-ASDP II) ilizinduliwa tarehe 4 Juni 2018na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. John Pombe Magufuli.Programu itatekelezwa kwa muda wa miaka kumi kuanzia mwaka 2017/18hadi 2027/2028 katika awamu mbili ambazo zimegawanyika katika vipindiviwili vya miaka mitano (5) kwa kila awamu. Awamu ya kwanza ya utekelezaji imeanza mwaka 2017/18 na kufikia mwisho mwaka 2022/23 naawamu ya pili ya utekelezaji itaanza mwaka 2023/24 na kufikia mwisho mwaka 2027/28. ASDP II ni mwendelezo wa utekelezaji wa Awamu ya Kwanza ya Programu ya Kuendeleza Sekta ya Kilimo iliyotekelezwa kwa miaka saba kuanzia mwaka 2006/2007 hadi 2013/2014. Hivyo maandalizi ya utekelezaji wa ASDP II yamezingatia mahitaji ya sasa ya nchi na ajenda ya kufikia uchumi wa kati na pia uzoefu uliotokana na utekelezaji wa awamu ya kwanza ya programu.
 

Download File/s: